Alhamisi , 6th Aug , 2015

Halmashauri ya manispaa ya Iringa imeanza kupunguza maambukizi ya virusi nya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa baada ya vijana kuanza kuhudhuria kliniki ya huduma rafiki kwa vijana zihusuzo afya ya uzazi na mtoto zinazotolewa katika zahanati mbalim

Washauri nasaa na upimaji wakimpima mkazi wa eneo la Mlandege Iringa.

Mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Dkt. Mei Alexander amesema hayo wakati alipopokea vifaa mbalimbali katika zahanati tano vilivyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la AMREF chini ya mradi wa afya ya uzazi ni haki ya kijana tuitetee.

Amesema mradi huo umekamilisha utoaji wa vifaa tiba pamoja na ukarabati wa majengo ya zahanati hizo ili ziendane na huduma rafiki zinazoweza kuwavutia vijana kuhudhuria kliniki hizo.

Akizungumza na kwenye zahanati ya kitwiru muuguzi mkuu wa zahanati hiyo Esther Sanga amesema wamefanikiwa kuongeza idadi ya vijana wanaohudhuria kliniki baada ya kuhamasisha vijana kwa kutumia mikutano ya hadhara hiyo ikiwa ni baada ya wahudumu wenyewe kupatiwa mafunzo yaliyofadhiriwa na shirika hilo la amref hali ambayo imesaidia siyo tu kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa bali pia mimba za utotoni.

Kwa upande wake meneja miradi ya afya uzazi mama na mtoto AMREF Benatus Sambili amesema shirika hilo liliamua kupeleka mradi huo wa miaka mitano wenye thamani ya dola milioni sita za kimarekani uliotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano katika halmashari za manispaa ya iringa,ilala na kinondoni baada ya kuona mahitaji ya maeneo husika na kwamba mradi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya vijana wanaopata huduma za afya ya uzazi.