Jumatatu , 29th Mar , 2021

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya Obama, katika kijiji cha Kogelo Kaunti ya Sia nchini Kenya, Mama Sara Obama ambaye amefariki leo Machi 29, 2021, atapumzishwa kesho Machi 30, 2021 asubuhi.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama

Mama Sara amesifiwa na wengi kama mtu aliyekuwa mkarimu, mpenda watu na mcha mungu ambapo Sheikh Musa Ismail wa Kaunti ya Sia amemwelezea.

Wakenya watamkumbuka mama sara kwa ukarimu na kujitolea kwake kutetea maslahi ya wajane na yatima, mwaka2014 akitunzwa na umoja wa mataifa kwa juhudi zake za kuboresha elimu kwa wasijiweza.

Bado haijabainika iwapo aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama atafika Kogelo kwa mazidhi ya mama Sara.

Zaidi tazama video hapo chini.