Jumamosi , 9th Jul , 2016

Viongozi wa Mikoa na Halmashauri zote nchini Tanzania wametakiwa kuhakikisha kwamba watumishi na waajiriwa wote ngazi ya mamlaka za serikali za mitaa wanahudhuria mafunzo ya namna bora ya kutoa huduma kwa wananchi wao.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na msemaji wa chuo cha mafunzo ya serikali za mitaa nchini LGTI bi. Orester Kilyenyi alipokuwa akiongea na East Africa Radio juu ya nama ambavyo chuo hicho kinalenga kuelimisha viongozi juu ya utendaji bora.

Bi Orester amesema, ni vyema kukawekwa utaratibu wa watumishi wa serikali kujikumbusha namna bora ya kushugulikia changamoto na kero za wananchi jambo ambalo litaongeza weledi na kuondoa watendaji wasio fuata sheria nataratibu za utumishi.

Adiha, Bi Orester amesema kuwa kwa mwaka wanazalisha watumishi 1500 licha kuwepo na hitaji kubwa la watumishi wa sekta mbalimbali katika halmashauri zote nchini ambapo amewataka wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu kujiunga na chuo hicho ili waweze kuitumikia serikali yao katika kiwango bora

"Mtu akijiunga na chuo chetu cha serikali za mitaa baata ya kuhitimu atapata ajira kwani watapangiwa moja kwa moja kazini chini ya serikali, unajua kwa sasa kuna almashauri mpya zimeanzishwa huko nako watumishi wanahitajika" amesema Orester