Jumatatu , 21st Nov , 2022

Wananchi wa kata ya Mtyangimbole halmashauri ya Madaba wilaya ya Songea mkoani Ruvuma wametoa zawadi ya mbuzi kwa viongozi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) 

Zawadi hiyo wameitoa baada ya wananchi hao kushuhudia utiaji wa saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa kata ya Mtyangimbole

Wananchi hao wameeleza kuwa tangu dunia iumbwe hawajawahi kupata maji safi na salama hivyo ujio wa mradi huo utaondoa adha hiyo ya upatikanaji wa maji katika kata hiyo