
Akitoa hukumu hiyo Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Dr. Adam Mambi amesema adhabu hiyo ni fundisho kwa vijana wengi wanaotumia njia za mkato kupata fedha zisizo za halali, na kusababisha mauaji yanayomaliza nguvu kazi ya taifa .
Awali akisoma shauri hilo mahakamani hapo Wakili wa Serikali, Shindani Michael, amesema washitakiwa wametenda kosa hilo Julai 25, 2014, eneo la Mpemba katika Halmashauri ya Mji Tunduma uliopo wilayani Momba mkoani songwe .
Amesema kuwa washitakiwa hao walimvamia marehemu Vascal Njowela, akiwa ametoka dukani kwake akielekea kwa bosi ili kuwasilisha mauzo, ambapo alikutana na watu hao watatu waliompiga risasi na kumkata kwa mapanga wakitaka kupewa Mil. 1.