Jumatano , 28th Oct , 2020

Wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt Hussein Mwinyi na Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari wamepiga kura hii leo visiwani humo, huku kila mmoja wao akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

Kushoto ni mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi na kulia ni mgombea urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha zoezi lake la upigaji wa kura Dkt. Mwinyi akatumia fursa hiyo kuwapongeza Wazanzibar wote waliojitokeza kupiga kura.

"Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe ambao hawajafika waendelee kujitokeza kupiga kura na hatimaye zoezi liishe kwa amani", amesema Dkt Mwinyi.

Kwa upande wake mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesema kuwa masuala ya kuwatoa mawakala katika vituo siyo sahihi kwani wakala anakuwepo mahala pale kwa lengo la kulinda kura za mgombea wake.