Ijumaa , 4th Dec , 2015

Halmashauri ya wilaya ya Njombe leo imefanikiwa kuwaapisha madiwani wake na kufanya uchaguzi wa mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo na makamu wake huku kamati za kudumu zikiundwa.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba

Baada ya kula kiapo na kuwa madiwani rasmi madiwani hao wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia mapato na makusanyo ya halmashauri hiyo ili kuhakikisha kuwa halmashauri inafanikiwa kuboresha maendeleo yake.

Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Njombe upande wa TAMISEMI Joseph Makinga amesema kuwa halmashauri hiyo ina shida katika ukusanyaji wa mapato na kushindwa kufikia malengo yake hivyo jukumu lao ni kuhakikisha kuwa wanasimamia ukusanyaji wa mapato.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba amesema kuwa madiwani hao wahakikishe kuwa wanasimamia vizuri mapato ya ndani na nje ya halmashauri hIyo ili kuimarika kiuchumi.

Hata hivyo baada ya kuchaguLiwa mwenyekiti wa baraza hilo Varentino Hongoli kwa kupata kura asilimia 94 ambapo waliopiga kura 18 na yeye kupata kura 17 huku kura ya hapana ikiwa ni moja.