Jumatano , 16th Nov , 2022

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametaka mafunzo ya masuala ya fedha kuendelea kutolewa wa wadau wa habari na wadau wa masuala ya fedha na uchumi, ili kuchochea maendeleo ya uchumi nchini.

Mkuu wa Habari East Africa TV na East Africa Redio, Barnabas Mkongwe akiwa na Mkuu Msaidizi wa Idara ya Habari ITV Isaac Mpayo

Naibu Waziri Kipanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa mahafali ya mafunzo maalum ya masuala ya fedha yaliyoratibiwa na Bloomberg Media Initiative Africa (BMIA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa wadau wa habari na wadau wa masuala ya fedha na uchumi.

Akihutubia katika mahafali hayo Naibu Waziri amehimiza mafunzo haya kuendelea kutolewa kwa waandishi na wadau wa masuala ya fedha wengine kwani yanatija katika kukua kwa uchumi wa Taifa letu. 

Mkuu wa Habari East Africa TV na East Africa Redio, Barnabas Mkongwe ambaye ni miongoni mwa wahitimu wa mafunzo hayo ameeleza kuwa mafunzo waliyoyapata watayatumia kuisaidia jamii kupata uelewa zaidi kuhusu masuala ya fedha na uchumi.

Kwa upande wake Bakari Machumu mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited na Mkuu Msaidizi wa Idara ya Habari ITV Isaac Mpayo wakawahimiza waandishi wengine kuchangamkia fursa mbalimbali za mafunzo.