Jumatatu , 10th Oct , 2022

Takribani watu 25 wamepoteza maisha huku wengine 50 wakiwa hawajulikani walipo baada  ya maporomoko ya udongo kuyakumba makazi yao  huko nchini  Venezuela katika mji wa  Las Tejerías.

Takribani vikosi  1,000 vya dharura vimewasili kwenye eneo la tukio ili kuendelea na uokoaji. 

Makamu wa Rais wa nchi hiyo Delcy Rodríguez amesema kwamba vikosi vya uokoaji vinajaribu kufanya uwezekano wa kuokoa kila mmoja huku pia akitoa pole kwa familia za waathirika.    

Naye Rais Nicolás Maduro wa  nchi hiyo ametangaza siku tatu za maombolezo kitaifa kufuatia tukio hilo.  Kati ya waliopoteza maisha wamo watoto wawili wadogo waliokua wakitambaa. Mvua kali nchini humo zimesababisha kupasuka kwa kingo za mto El Pato  na kupelekea mafuriko makubwa.