Jumamosi , 3rd Sep , 2022

Takribani watu wawili wamepoteza maisha nchini Uganda huku mwingine mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya kutokea kwa mafuriko makubwa  katika wilaya ya  Bundibugyo  usiku wa jana.

 Mvua iliyonyesha kwa zaidi ya saa 6 imesababisha hasara kubwa kwenye makazi ya watu haswa kwa kuharibu nyumba na mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi.  Mchana wa leo mwili wa mtoto mmoja mwenye umri wa miak 4  aitwae  Pritha Masika ulipatikana.

Mtoto  huyo alifariki dunia majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo akiwa kwenye nyumba ya baba yake katika kijiji cha  Kubango , ambapo mvua kubwa ilimkuta amelala na kumsomba na maji na kufukiwa na udongo.