
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Rais Magufuli amesema hayo leo Disemba 28, 2018 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), vyama shiriki, watendaji wakuu wa mifuko ya Hifadhi ya jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) ili kujadili kwa pamoja kuhusiana na mjadala wa kikokotoo kipya cha mafao kwa wastaafu.
"Formula nzuri ni zile zinazo wapromote wafanyakazi, ndio ninazozitaka mimi, formula zinazowanyima haki wafanyakazi sio formula nzuri, ninashukuru katika kipindi hiki kifupi cha kuunganisha mifuko tumeanza kuona matokeo", amesema Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa, "Mifuko hiyo itakuwa imetengamaa, ni matumaini yangu, nitaichungulia kweli kweli hiyo mifuko, na Waziri natoa maagizo yake, wachungulie kweli, ili kusudi watu wasitumie hovyo hovyo, hii ni mifuko ya wanachama".
Hivi karibuni uliibuka mjadala huo baadaya Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kutoa kikokotoo kipya ambacho kilikuwa kikitaka mstaafu wa sekta ya Umma kupatiwa asilimia 25 ya mafao yake kwa mkupuo badala ya ile 50 ya mwanzo.