
Mabehewa ya abiria yaliyoanguka
Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani, amesema hali ya majeruhi waliowengi maendeleo yao ni mazuri na wengine wameruhusiwa kabisa kutoka katika hospitali ,huku akitaja majeruhi 6 wenyewe wamesafirishwa kwenda mkoani Mwanza.
Hata hivyo zoezi la kuwasafirisha abiria zaidi ya 900 walionusurika katika ajali ya Treni hiyo hapo jana ambayo ilikuwa ikitoka mkoa wa Kigoma kupitia Tabora mpaka Dar es Salaam, limefanyika usiku wa jana huku chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni kukatika kwa kipande kimoja cha reli na hivyo kusababisha mabehewa 8 ya abiria kuanguka .