Makamba kutoa milioni 80 kwa mikoa mitatu

Jumatano , 15th Mei , 2019

Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, ametangaza neema kwa mikoa nchini itakayoibuka kidedea katika kupiga vita mifuko ya plastiki.

Waziri January Makamba

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Makamba amesema kuwa ameshazungumza na wakuu wote wa mikoa juu ya mkakati wa kufanikisha marufuku hiyo ya mifuko ya plastiki na kuwaahidi zawadi kwa mkoa utakaoibuka mshindi pamoja na mkoa wa pili na wa tatu.

Serikali imetangaza marufuku ya mifuko ya plastiki kuanzia Juni mosi, na kusisitiza kuwa atakayevunja sheria hiyo, atakumbana na adhabu kali.

Tazama video hapa chini.