Alhamisi , 28th Apr , 2016

Mwili wa Mwanamuziki nguli wa DRC Papa Wemba umewasili nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo kutokea Ivory Coast ambapo mauti yalimfika akiwa kazini nchini humo.

Mamia ya raia wa DRC leo wamejitokeza kwa wingi katika uwanja wa Kinshasa kuweza kuupokea mwili wa mwanamuziki huyo aliyependwa sana kutokana na mchango wake wa muziki katika nchi hiyo na mataifa mengine duniani.

Mwanamuziki huyo ambaye ametajwa kuwa mmoja ya waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya cha Soukous anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya mwili huo kuwekwa katika uwanja wa mpira kwa raia kutoa heshima zao za mwisho.

Aidha mwanamuziki huyo alienda Abdjan Ivory Coast tamasha la bure la usiku kucha lilifanyika mjini Abidjan ambapo mwanamuziki huyo alianguka alipokuwa akiimba.Mashabiki wengi walivalia nguo nyeusi na kubeba mishumaa ili kutoa heshima kwa nguli huyo wa muziki.

Chanzo BBC