Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limepiga marufuku kupiga fataki bila Kibali katika msimu wa sikukuu za Christimas na Mwakampya.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Dec 24 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP AUGUSTINO SENGA amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yote ya mkoa yatakayokuwa na mikisanyiko.
Kamishna Senga ameongeza kuwa milango iko wazi kwa watu wenye nia ya kupiga fataki kuomba Kibali masaa 24 kabla ili jeshi hilo liweze kusimamia zoezi la upigaji wa Fataki.

