Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Mwamri ametoa agizo mara baada ya kukagua madawati katika shule ya msingi ya Kitongo katika halmashauri ya mji wa Nzega na kubaini karibu madawati 18 yote yametengenezewa mabaki ya mbao yanayojulikana kama mabanzi.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye licha ya kuyakataa madawati amesema ataendelea kufanya hivyo kwa madawati mingene ambayo atagundua yametumia mabaki hayo huku akisisitiza kuwa serikali inatumia gharama nyingi katika kulipia madawati hayo.
Aggrey Mwanri akatumia fursa hiyo kuwataka vingozi wa Halmashauri hiyo kuzingiatia agizo lake hilo na kusema kuwa haiwezekani Tabora kuwa mkoa unaozalisha magogo kwa wingi na kuuza nje ya mji huo wakati watoto wanakaa chini na madawati yanayotengenezwa chini ya kiwango.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt. Thea Ntara, amesema kuwa atahakikisha kuwa yeye na watendaji wake weatasimamia zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili kupata madawati yenye viwango na ambayo yatadumu kwa muda mrefu.