Jumamosi , 17th Nov , 2018

Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, kutengua uteuzi wa waliokuwa mawaziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage pamoja na aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Charles Mwijage wawili hao waliibuka bungeni wiki hii.

Waliokuwa Mawaziri Charles Mwijage na Charles Tizeba.

Wawili hao ambao walikuwa watu wa karibu kupitia taasisi za wizara zao, waliuliza maswali bungeni kwa nyakati tofauti maswali ambayo yalikuwa wakiuliza  kwa waliolkuwa wajumbe wenzao kwenye baraza la Mawaziri lakini wao wakiwa kama wabunge wa majimbo yao husika.

Novemba 13 aliyekuwa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba, alihudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma na kushangiliwa na Wabunge, pale Naibu Spika Tulia Ackson alipomtaja ili kuuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Dkt. Tizeba ambaye pia ni Mbunge wa Buchosa, alisimama na kupigiwa makofi na wabunge wenzake, kisha akamuomba Naibu Spika kumruhusu kusema maneno mawili tu, na kusema kwamba.

La kwanza ni kumshukuru sana Mh. Rais Magufuli kwa Fursa aliyokuwa amenipa ya kulitumikia taifa, lakini pia nikushukuru wewe na Mheshimiwa Spika kwa ushirikiano nilioupata wakati nikitumika serikalini ndani ya Bunge lako”.

Kauli hiyo iliendelea kupigiwa makofi na Wabunge wenzake, na kisha akauliza swali alilokusudia, ambalo lilihusu ujenzi wa vivuko vilivyomo kwenye jimbo lake la Buchosa.

Novemba 16 aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage ameibuka na kuzungumza bungeni, kwa mara ya kwanza tangu atenguliwe nafasi yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wiki iliyopita.

Akizungumza Bungeni Jijini Dodoma kabla hajauliza swali kwa Wizara ya Nishati, Mwijage amelishukuru bunge hilo kupitia kwa Spika Job Ndugai wakati wote wa Uwaziri wake ndani ya Bunge.

Nawashukru sana tangu mlivyokuwa mkiniongoza bungeni, kupitia kwako Mwenyekiti napenda kumshukuru Rais,  Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa namna ambavyo waliniamini na kunisimamia kwenye majukumu ambayo walinipa.”

Wiki iliyopita, Rais Magufuli alipokuwa akiwaapisha mawaziri wapya wawili na naibu mawaziri wanne, alibainisha kuwa Charles Mwijage, na Charles Tizeba walishindwa kufanya maamuzi wakati wafanyabiashara wa korosho waliposhindwa kununua korosho za wakulima.

"Nilimwambia Waziri Mkuu awakumbushe mawaziri wake, kwa sababu matatizo mengi yaliyokuwa yakihusu kilimo na viwanda yalikua yanamalizwa na Waziri Mkuu, nilijiuliza pia kahawa ni kilimo pia vipi Waziri hakuliona pia." Rais Magufuli.

"Nilijiuliza kwanini hawa tuliowapa, majukumu hawafanyi hivi, ni ukweli pia bei ya soko la korosho limeshuka kidogo unapoona kuna tatizo unamtuma Waziri Mkuu anatatua," aliongeza Rais Magufuli.