
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bakar Hamad Bakar
Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 24, 2023, Bungeni jijini Dodoma, wakati akichangia mara baada ya Waziri Jafo kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23
"Haiwezekani mwananchi amesafiri kutoka Zanzibar na kg 2 za sukari, TV used moja anakuja kutumia nyumbani anafika Bara anaambiwa alipe kodi, hii ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzabnia ni nchi moja haiwezekani anayetaka Morogoro kwenda Dar es Salaam halipi kodi, lakini anayetoka Zanzibar kuja Bara akifika Dar es Salaam anatakiwa alipe kodi, hii ni kero kubwa," amesema Mbunge Bakar
Aidha akaomba ufafanuzi pia kwenye magari "Tunaona magari ya nchi mbalimbali yanayozunguka hapa Tanzania hayaletewi usumbufu wowote lakini kuna changamoto kubwa kwa usajili na utambuzi wa gari zinazotoka Zanzibar kuja Bara kuweza kutumika hapa, Tanzania ni moja kwanini mpaka leo hakuna sheria inayosajili gari kutoka Zanzibar kuja kutumika Bara?,"- Bakar Hamad