
Mbunge wa Tanga aliyemaliza muda wake, Mussa Mbarouk
Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahojiano na EATV na kusisitiza kuwa kwa dhati ya moyo wake, anakipongeze Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa kuhakikisha watu hao hawarudi kwani hii itakuwa fundisho kubwa kwa watu wenye tabia za kuhamahama.
"Wanaosema CUF imekufa ni wale waliokuwa na nia ovu na chama chetu, sasa wametoka na kuhamia vyama vingine, wale walioenda CCM mnajua kilichowatokea maana wenye chao hawakukubali kukaribisha wageni kwa sababu wapo waliokipatia tabu chama chao, mimi nawapongeza CCM kwa kuwapiga chini wale Madiwani waliotoka CUF na kuhamia CCM", amesema Mbarouk.