Ijumaa , 21st Oct , 2022

Meya wa jiji la Arusha Maxmilan Iraqhe ametoa onyo kwa  mtu yeyote atakaebainika kutoa taarifa za uzushi zinazolenga  kuchafua  hadhi ya halmashauri ya jiji hilo hasa katika upande wa mapato kwani kwakufanya hivyo ni kinyume cha taratibu zilizowekwa

Meya Iraqhe anabainisha kuwa kumekuwa na taarifa za upotoshaji katika mitandao  kuhusu hali ya mapato katika jiji hilo, jambo ambalo sio sahihi ambapo anasisitiza kuwa hawatasita kumchukulia hatua za kisheria kwa atakaebainika anafanya hivyo

Katika hatua nyingine Iraghe anatoa angalizo kwa watumishi wanaofanya vitendo vya  ubadhirifu  fedha za miradi mbalimbali ikiwemo ya afya na elimu ambayo imewekwa kwa manufaa ya wananchi

Haya yanajiri ikiwa jiji hilo limefanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa kipichi cha  Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2022-2023 shilingi billion saba nukta tano tisa nane ikiwa ni  ongezo la zaidi ya bilioni moja nukta tatu