Mghwira amrithi Meck Sadick

Jumamosi , 3rd Jun , 2017

Aliyekuwa Mgombea urais 2015 kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo Bi Anna Elisha Mghwira ameteuliwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Taarifa kutoka ikulu imesema kuwa Bi Anna Mghwira ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Taifa anaenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadick aliyekubaliwa kujiuzulu na Mh. Rais tar 16 Mei mwaka huu.

Pamoja na hayo Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor, pamoja na DIGP Abdulrahman Omar Juma Kaniki kuwa Mabalozi na kwamba tarehe ya kuapishwa itatangazwa.

Barua ya uteuzi kutoka Ikulu.