Ijumaa , 27th Mei , 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, ameawataka Watanzania kushiriki na kujifunza namna ya utengenezaji wa bidhaa zenye ubora wa viwango kupitia maonyesho ya bidhaa mbali mbali kutoka nchini Misri.

Profesa Mkenda, amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa maonyesho hayo ya bidhaa kutoka nchini Misri ambayo pamoja na mambo mengine yana lengo la kuvutia uwekezaji hapa nchini.

Kwa upande wao wafanyabiashara waliokuja kuonyesha bidhaa zao katika maonesho hayo wamesema kuwa wamevutiwa sana na mazingira ya kibiashara nchini hivyo wanahitaji ushirikiano wa pamoja na wafanyabiashara wa ndani ili waweze kufanya biashara pamoja.