Ijumaa , 3rd Jul , 2020

Ajali ya gari imeuwa watu watano na kujeruhi wawili, baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma kugongana na lori huko Kibaigwa Dodoma.

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Julai 2, 2020 katika barabara kuu ya Morogoro - Dodoma.

Aidha Kamanda Muroto amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori.

''Ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa lori ambaye aliingia katikati ya barabara akitokea kwenye kituo cha mafuta bila kuangalia pande zote za barabara na kusababisha Noah kuingia uvunguni mwa lori'', amesema Muroto.

Pia ameeleza kuwa dereva wa lori ametoroka na jeshi la polisi linaendelea kumsaka huku likifanya uchunguzi zaidi wa ajali hiyo.

Kuhusu majeruhi wawili wa ajali hiyo Muroto amesema mmoja ana hali mbaya zaidi na juhudi za madaktari zinaendelea katika kunusuru uhai wake.