Jumatano , 10th Jul , 2024

Mkuu wa Shule ya sekondari Kiteme Charles Mkaruka (33) amesimamishwa ukuu wa Shule na Halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoani Kagera ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili baada ya kumuadhibu Mwanafunzi wa kidato cha tatu (jina limehifadhiwa) na kumjeruhi sehemu mbalimbali

za mwili wake kwa kosa la kukataa kusoma somo la Phizikia

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Muleba Abel Nyamahanga ambapo wamesema kuwa wamemvua madaraka ya ukuu wa Shule mwalimu huyo ili kupisha hatua za kiuchunguzi.

Awali akielezea tukio hilo Mwanafunzi huyo amesema kuwa alimuelezea mkuu wa Shule kuwa somo hilo haliwezi ila akamlazimisha.

Mwalimu huyo ameachiwa kwa dhamana na Mwanafunzi ameruhusiwa kutoka kituo cha afya Kemeya baada ya Afya yake kuendelea kuimarika.