Jumanne , 22nd Mar , 2016

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ameunda kikosi kazi cha wanne kwa ajili ya kufanya uhakiki wa wafanyakazi hewa katika halmashauri zote za Mkoa wa Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri ameunda kikosi kazi cha wanne kwa ajili ya kufanya uhakiki wa wafanyakazi hewa katika halmashauri zote za Mkoa wa Tabora.

Mwanri amesema kikosi kazi hicho kimepewa hadidu za rejea ambazo pia zitaainisha idadi ya wafanyakazi waliostaafu, walioachakazi, waliofukuzwa na waliohama ili kujua kama kuna mishahara hewa inalipwa na ni kwa nani.

Akizungumza na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo, Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa halmashauri itakayobainika ina watumishi hewa na mishahara yao inaliwa basi wakuu wa idara husika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Katika hatua nyingine Agrey Mwanri ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Uyui kwa kuanza kutekeleza agizo la kuwabaini watumishi hewa kwa kufanya ukaguzi kwa watumishi wake wote wa Halmashauri hiyo ambao ni 2400.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi amesema ujio wa Mkuu wa mkoa kwa mara ya kwanza katika wilaya hiyo ni ukombozi Mkubwa kwao kutokana na halmashauri hiyo kusahaulika na viongozi wa juu.