Jumatano , 15th Mar , 2023

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya CHADEMA Slyvester Kanyasi Masinde, amefariki dunia leo Machi 15, 2023 katika hospitali ya rufaa ya Bugando Mwanza alikokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu. Mzee Masinde pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa CHADEMA.

Slyvester Kanyasi Masinde, wakati wa uhai wake

Kufuatia taarifa hiyo CHADEMA imetoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na wajumbe wa bodi ya udhamini ya chama hicho, na kwamba taarifa za kina juu ya mazishi zitatolewa baadaye.