
Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari imesema mabadiliko hayo yamelenga kuwawezesha wabunge kujifunza, kujipatia uelewa na uzoefu zaidi katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kamati za Bunge.
Taarifa hiyo imesema kuwa wabunge wote waliokuwa wajumbe wa kamati ya masuala ya UKIMWI, hapo awali wamepangiwa kamati nyingine kwa nia ya kuboresha utekelezaji wa majukumu ya kibunge.
Kwa mujibu wa waraka ulitolewa na Mhe. Spika mabadiliko hayo yataanza kutekelezwa mara moja kuanzia mwezi huu wa Oktoba 2016 ambapo wajumbe husika watakutana kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wao na kuandaa ajenda za vikao vya kamati.