Neno la Ndugulile baada ya Mollel kuteuliwa

Jumapili , 17th Mei , 2020

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile ameeleza kushukuru uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli juu ya kumtengua na nafasi yake kuijaza Mbunge wa Siha,Godwin Mollel.

Dkt. Mollel ambaye ametuliwa kuwa Naibu Waziri Mpya wa Wizara ya Afya na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Ndugulile ameandika ujumbe pia wa kumpongeza Dkt. Godwin Mollel kwa kupewa nafasi hiyo.

"Nimepokea uamuzi wa Rais Magufuli kwa unyenyekevu mkubwa, ninamshukuru sana kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika Serikali yake. nawashukuru sana Ummy mwalimu na watendaji wote kwa ushirikiano walionipatia, namtakia kila la kheri Naibu Waziri ajaye Dkt. Godwin Mollel." Faustine Ndugulile aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya."

Jana Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Afya Faustine Ndugulile na kumteua Godwin Mollel ambaye ni Mbunge wa Siha kushika nafasi hiyo.