Jumanne , 4th Oct , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameyataka mashirika na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali zinazopewa vibali vya kuendesha majukumu yake Tanzania, kufanya kazi inazoainisha katika usajili wake ili kuisadia nchi kufikia malengo yake iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kuiunganisha nchi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa maagizo hayo leo Oktoba 4, 2022, Jijini Dodoma kwenye jukwaa la mwaka la mashirika yasio ya kiserikali na uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa uendelevu wa mashirika yasiyo ya kiserikali NSNS.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa, ameyaagiza mashirika kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kuchukua changamoto zinazotolewa na wananchi na kuzipatia majawabu.