
Mama Mzazi wa Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera, Verdiana Mjwahuzi, wakati wa uhai wake.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa msiba wa Mama Erick Kabendera, utakuwa maeneo ya Tabata Chang'ombe karibu na maduka mawili.
Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Mama huyo, alijitokeza hadharani mbele ya Waandishi wa Habari siku ya Disemba 13, mwaka huu na kumuombea msamaha mwanaye anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, amsamehe mwanaye ili arudi nyumbani kumuuguza.