Jumatatu , 27th Dec , 2021

Kijana Daniel Joseph, ameeleza namna mwaka 2014, ulivyobadilisha maisha yake baada ya kupigwa na waya wa umeme wakati akitokea shambani kumsaidia rafiki yake kubeba mahindi, hali ambayo imempelekea sura yake isiwe ya kawaida.

Daniel Joseph

Akizungumza wakati wa Shangwe za Krismasi, Daniel alisema kwamba hapendi watu wamuonee huruma, na anachokihitaji kwa sasa ni msaada kwa ajili ya kupata pesa ili aweze kuwa na sehemu ya kutengeneza sofa na kuanza maisha sababu analala kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.

Mwonekano wa sura ya Daniel umepatikana baada ya kufanyiwa oparesheni mara 37, na namba ya kumsaidia ni  0769 228 230