
Aidha jumla ya pikipiki 12 zimekamatwa huku mbili kati ya hizo zikikuwa hazina namba za usajili badala yake zilikuwa na plate namba iliyosomeka R.I.P SCOBER.
Polisi wanasema watumiwa hao wamehojiwa kwa kina na kukiri kufanya matukio ya uporaji, ukabaji na kujeruhi watu kwa kutumia pikipiki hizo katika maeneo tofauti tofauti katika mkoa huu na wametaja mtandao mzima wa wahalifu wanaoshirikiana katika matukio hayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo ametoa wito kwa wananchi hususani wazazi na walezi kuendelea kuwapa malezi mema nakuwaonya vijana wao ili kuepusha kutojiingiza katika uhalifu na uvunjifu wa sheria za sheria za Nchi, pamoja na wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi