Ijumaa , 24th Dec , 2021

Jeshi la Polisi Arusha katika kusherehekea sikukuu za Krismasi, limewataka wamiliki wa bar kuzingatie masharti ya leseni zao zinaonesha muda wa kufunga na kwamba wamiliki wa kumbi na maeneo ya starehe wahakikishe hawajazi watu kupita kiasi kwa sababu za kiafya ikiwamo tahadhari ya Corona.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo.

Taarifa hiyo imetolewa leo Desemba 24, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, na kupiga marufuku wazazi kuwapeleka watoto wao kwenye majumba ya starehe na vileo.

Aidha, madereva pia wamepigwa marufuku kuendesha gari wakiwa wamelewa na mwendokasi na kwa wale watakaobainika kufanya hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.