Jumanne , 4th Feb , 2020

Rais wa Jamhurti ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ametuma salamu za pole kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Pili wa nchi hiyo Daniel Arap Moi aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Pili wa Kenya Daniel Arap Moi

Taarifa za kifo hicho zimetangazwa alfajiri ya leo Februari 4, 2020 na Rais Uhuru Kenyatta, ambapo Moi amekuwa akiugua kwa muda na mara kwa mara amekuwa hospitalini, licha ya kuwa mwenye afya nzuri baada ya kipindi chake cha Urais.