Jumapili , 7th Nov , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtaka Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Visiwa vya Comoro Mhe. Pereira Ame Silima kuratibu vizuri usafiri wa meli kati ya Tanzania na visiwa hivyo kwa kuwa wanategemea Tanzania kwa kila kitu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan, ameyasema hayo wakati akimuapisha Mhe. Pereira Ame Silima kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Visiwa vya Comoro leo tarehe 07 Novemba, 2021 Ikulu, Chwamwino Mkoani Dodoma.