
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Rais Samia ameyasema hayo leo wakati wa maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge Mkoani Kagera, huku pia akizitaka taasisi hizo zenye dhamana ya kuzuia na kupambana na rushwa pia kujichunguza pia.
“Vyombo tulivyoviamini TAKUKURU NA ZAECA kabla hamjaenda kushughulikia taasisi nyingine naomba mjipekue ndani kwenu kwanza“ - Amesema Rais Samia Suluhu Hassan
Aidha Rais Samia amewataka watanzania kuendelea kumuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa kufanya yale aliyoyahimiza na kuyaacha yale aliyokuwa akiyapinga ikiwa pamoja na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Kwa takribani siku 195 Mwenge wa Uhuru umekagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 1293 yenye thamani ya shilingi bilioni 650.8 ambapo miradi ya setka ya maji imetajwa kufanya vizuri kuliko miradi ya sekta nyingine katika utekelezaji wake.