Alhamisi , 19th Mei , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka Mawaziri wa Wizara zote nchini kutokuogopa maneno badala yake wachape kazi kwa maendeleo ya nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Maagizo hayo ameyatoa hii leo Mei 19, 2022, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi pamoja na mambo mengine amesema vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi mkoani Tabora, ameamua kwamba vibaki mahali vilipo na mipaka ya hifadhi hizo ameisogeza nyuma.

"Niwatie moyo mawaziri wangu January, Bashe, Aweso, Bashungwa, Mbarawa akina Mwigulu na wengine wote, chapeni kazi kwa maendeleo ya nchi, kuna weza kukawa na maneno mengi sana, lakini hampati kama yale ninayoyapata mimi kiongozi wenu lakini hayanivunji moyo najenge nchi," amesema Rais Samia