Ijumaa , 4th Nov , 2022

Rais wa Guinea  Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa muda wa  miaka 43, amezindua azma yake ya kuwania tena muhula wa sita wa kuwa raia wa nchi hiyo.

Rais Obiang anaiongoza Guinea tangu mwaka 1979

Bw Obiang, mwenye umri wa miaka 80, alitwaa madaraka mwaka 1979 kutoka kwa Rais Francisco Macias Nguema, ambaye alikuwa kiongozi wakati wa uhuru  ambaye utawala wake ulikuwa wa ghasia zilizopelekea vifo vya watu wengi.

Uchaguzi mkuu wan chi hiyo umepangwa kufanyika Novemba 20 mwaka huu.

Rais huyo aliuambia mkutano wa hadhara kwamba chama chake kimemchagua kugombea "kwa sababu yeye  ni ishara ya amani inayotawala Guinea ya Ikweta",  

  nchi hiyo ina jumla ya  wapiga kura 425,000 waliojiandikisha kati ya idadi ya watu wapatao milioni 1.4