Alhamisi , 8th Dec , 2022

Bunge la nchini Peru limemuondoa madarakani Rais wa taifa hilo Pedro Castillo na nafasi yake kuzibwa na makamu wa Rais Dina Boluarte baada ya Rais huyo kufanya jaribio la kuvunja bunge la nchi hiyo

Rais huyo alitangaza kutaka kulivunja bunge la nchi hiyo baada ya bunge kuanza mchakato wa kupiga kura za kumuondoa Rais huyo kwa kile wanachodai kuwa sio muadilifu kazini

Katika zoezi la kura wabunge 101 walipiga kura za ndio. na hapana 6 huku kura 10 zikiharibika