Jumatatu , 16th Jan , 2023

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka watanzania kupuuza uvumi wa watu ambao wanasema ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi maarufu kama daraja la JPM uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 700 umesimama

RC Malima amefika kujionea maendeleo ya ujenzi wake na kuwaonya wanaosambaza uvumi kwamba ujenzi wake umesimama

"Hili daraja kwa ukubwa wake watu walianza kuleta maneno kidogo eti litamshinda mama ila halijamshinda mama anaupiga mwingi sana na daraja limefikia asilimia 63 limechelewa sababu ya vitu viwili moja huko vinakotoka huko China kulikuwa na COVID - 19 ndio vikachelewa na uzalisha wake huko China ukapungua na ratiba nyingine zikabadilika" 

Katika hatua nyingine RC Malima ametoa onyo kwa watakaojihusisha na wizi wa vifaa katika daraja hilo na kwamba kwa atakayebainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake

‘Tumekaa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, viongozi wa tanroads pamoja na mkandarasi nimewahakikishia kwamba watu waendelee kudokoa kama wanataka lakini tutakapowakamata hilo litakalo wapata wasilalamike kwa sababu huyo sasa tutaingia ane vitani ni adui wa Tanzania wewe unaiba darajani unaona unamuibia mtu mchina wakati daraja Ietu sisi’

Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Mwanza Ambrose Paschal amesema mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana na wanatarajia ujenzi wake utakamilika kwa wakati

"Wasio na nia njema wanasema ujenzi umesimama lakini tunafanya ukaguzi wa mara kwa mara na mkandarasi anafanya kazi usiku na mchana na tunatarajia kukamilisha ujenzi wake kwa muda uliopangwa"