
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza na wanahabari na wafanyabiashara baada ya kutembelea soko la Vetenary
RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.
Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO, Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.