
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea miradi wa maji wa Mgango, kiabakari, Butiama miradi ambao ulitakiwa kukamilika mwezi huu wa desemba lakini mpaka sasa mradi huo upo asilimia 70 za utekelezaji wake huku mkandarasi mshauri akitupiwa lawama za kuwa chanzo cha ucheleweshwaji wa mradi huo
Akizungumiza mradi huo wa maji Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mgango, kiabakari, Butiama amesema ujenzi huo umesogezwa mbele kutokana na kuchelewa kwa pampu za kusukuma maji toka ziwani kwenda katika matanki
Mradi huo wa maji unategemea huhudumia zaidi ya wakaazi laki moja ndani ya vijiji 16 kwa awamu ya kwanza na utakapokamilika utafikia jumla ya vijiji 39 mkandarasi anaetekeleza mradi huu ni kampuni ya Unik Costaraction kutoka nchini Lethoto.