kama Mahakama ilivyoelekeza na kwamba elimu hiyo inapaswa kutolewa kwa wasichana wote, ambao ndio wahanga wakubwa wa suala hilo na jamii kwa ujumla.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Oktoba 24, 2019, ikiwa ni masaa machache tu tangu Mahakama ya Rufani, ilipokubali kuwa vipengele namba 13 na 17 vya sheria ya ndoa ya mwaka 1971, vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kuolewa ni batili na vinapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
''Bunge limepewa mwaka mmoja wa kubadilisha hiyo Sheria, sisi kama wananchi ni kuhakikisha maamuzi ambayo yametolewa yanaweza yakatekelezwa na Bunge likafanya kazi yake ndani ya huo muda wa mwaka mmoja uliolekezwa na Mahakama, kazi ya kumaliza ndoa za utotoni inahitaji sheria na jitihada zingine na tutaendelea kufanyakazi na jamii na wasichana kwakuwa ndio kwenye matokeo makubwa kwa kuhakikisha kabisa wasichana hawaozeshwi wakiwa na umri mdogo'' amesema Rebeca Gyumi.
Aidha Mwanaharakati huyo ameiomba jamii ya watanzania, kuhakikisha wanasimamia sheria hiyo kwa pamoja na kuifanyia kazi kwa sehemu kubwa ili kuhakikisha vikwazo walivyokuwa wanakumbana navyo wakati wa kutoa elimu vijijini vinakwisha kabisa.

