
Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda Mkondya amesema wakazi wa Mtwara ni watulivu na pia wanatii sheria, kwani mpaka sasa hakuna sehemu yeyote kwa wilaya zote za mkoa huo kulikoripotiwa tukio la uhalifu au uvunjaji wa sheria.
"Mtwara tunashukuru Mungu tumesherehekea sikukuu kwa amani, hakuna ripoti ya tukio lolote katika wilaya zote za mkoa huu, unajua wananchi wa Mtwara ni watu wanaopenda kutii sheria, ni watu wastaarabu, hivyo wamesherehekea kwa amani kabisa", amesema Kamanda Mkondya.
Hivi karibuni Jeshi la Polisi lilitoa tahadhari kubwa kwa wananchi kuwa makini na kutii sheria katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka, huku wakipiga marufuku kwa disco toto ambalo mara kwa mara kumekuwa kukitokea matukio yanahatarisha maisha ya watoto.