Jumatatu , 22nd Oct , 2018

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ametaja sababu ya kutodahiliwa zaidi ya wanafunzi 600 waliokuwa wametuma maombi yao ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kusema suala hilo limetokana na chuo kikuu hicho kupeleka idadi ya wanafunzi ambao haiendani na

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Pro Joyce Ndalichako

na mahitaji ya chuo hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Prof Ndalichako amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema ameagiza Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam na Tume ya Vyuo Vikuu nchini kukutana kwa pamoja kushughulikia suala hilo.

TCU ndio wanaoratibu zoezi la udahili wa vyuo vikuu, Chuo Kikuu cha Dar es salaam kilikuwa kimepeleka idadi ya wanafunzi ambao ni ndogo kuliko idadi ya wanafunzi wanaowahitaji, lakini siku  ya jumamosi nilizungumza na Mtendaji Mkuu wa TCU nikawaambia wakae Mkuu wa chuo ili waangalie na wanafunzi hao waliositishiwa udahili warudiswe. ” Amesema Profesa Ndalichako

Aidha Profesa Ndalichako amesema “nina mkutano leo kwenda kuangalia utekelezaji wa maagizo yangu, na ninarudia kusema kwamba UDSM ni ndotona matamanio ya wanafunzi. Na kwa mujibu wa  Mkuu wa Chuo, mpaka jumamosi walikuwa na nafasi 3000, hatupendi kuona wao taasisi za serikali halafu wanaendesha malumbano yasiyokuwa na tija.”

Hivi karibu kulisambaa taarifa juu ya usitishwaji wa udahili wa wanafunzi 682 ambao walikuwa wamepangiwa kujiunga masomo yao kwenye Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa sababu ya chuo hicho kufikisha idadi ya wanafunzi wanaohitajika.