Ijumaa , 21st Jan , 2022

Aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, wakati akiendelea kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, amedai kwamba hakuwahi kupewa haki ya kusikilizwa juu ya tuhuma zinazomkabili badala yake alivamiwa na kutengenezewa kesi ya uongo.

Lengai Ole Sabaya

Hayo yamejiri hii leo Januari 21, 2022, wakati mshtakiwa huyo wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Sabaya na wenzake sita akiendelea kutoa ushahidi wake mahakamani hapo.

Lengai ole Sabaya pamoja na wenzake katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi wanakabiliwa na tuhuma za kuchukua kiasi cha shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso kwa madai kwamba amekwepa kodi