Jumatano , 9th Apr , 2014

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amewahahakikishia Watanzania kwamba serikali ipo katika hatua za mwisho za kuandaa sera itakayosimamia sekta ya mafuta na gesi kwa ajili ya uwekezaji wenye tija kwa nchi.

Mabomba ya gesi yakiwa yamewasili katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka mikoa hiyo ya kusini hadi jijini Dar es Salaam

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la siku mbili la uzinduzi wa ripoti ya mwaka ya Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Umasikini nchini, REPOA Dk. Kikwete amesema hadi mwezi Oktoba mwaka huu serikali itakuwa imeweka utaratibu na sera kwenye sekta ya mafuta na gesi.

Dk. Kikwete amesema kwenye uwekezaji wa mafuta na gesi nchini utakuja na manufaa makubwa ya mabilioni ya fedha na hivyo ni nafasi muhimu kwa Watanzania wenye biashara za kati kunufaika na uwekezaji huo.

Kwa Upande wake Mtendaji mkuu wa REPOA,Profesa Samwel Wangwe amesema mategemeo ya Sera hiyo ya Mafutra na Gesi ni kuongeza ajira nyingi kwa vijana.