Alhamisi , 2nd Mar , 2023

Wataalam wa afya wameiomba Serikali na wadau kufanya uwekezaji mkubwa katika vifaa ambavyo vitaweza kubaini vinasaba ambavyo vitasaidia kutibu magonjwa mbalimbali ambapo kwa sasa takribani dola za kimarekani bilion 800 hutumika katika kutibu nje magonjwa hayo.

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi mkuu kutoka NIMR Prof Said Aboud katika mjadala wa pamoja uliowakutanisha madaktari,manesi,wadau wa aafya ukilenga kuongeza uelewa ili kuleta mabadiliko katika sera katika magonjwa adimu kama sikoseli,lupas na mengine.

"lazima tuangalie upya sera zetu ili tufanye uwekezaji mkubwa wa kuandaa wataalamu na vifaa ambavyo vitabaini vina saba hii itatusaidi kutibu magonjwa mengi"Prof Said Aboud

Akieleza umuhimu wa Vinasaba kwa wataalam na wananchi Prof Raphael Sangeda amesema madaktari wakipata uelewa wataweza kutibu magonjwa kwa kutumia vinasaba akisisitiza uwekezaji wa vifaa watalamu na mafunzo.

Aidha rais wa THGO amesema lengo ni kuwekeaa nguvu katika madakatari na manesi kufanya ugunduzi wa magonjwa adimu ambapo hali inaonesha kwa sasa uhitaji ni mkubwa kwenye eneo la vinasaba

'sasa hivi tunafanya mkakati ili madaktari wetu waaeze kumjua mgonjwa mwenye maradhi ya kurithi mfano sikoseli na mengine kwa sasa vipimo hivyo hadi kutumia maabara za serikali'Amesema Dkt Siana Nkya

Licha uwepo wa uhitaji mkubwa kwa baadhi ya wananchi kufahamu umuhimu wa Vina saba bado uwekezaji wake ni mdogo.