
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani, ametoa kauli hiyo katika mahafali ya Chuo cha Misitu Olmotonyi ambapo amesema ujangili wa misitu umekithiri katika maeneo mbalimbali na kulazimu kuundwa kwa jeshi hilo litakalosaidia kudhibiti uhalifu.
Aidha Mhandisi Makani, amezungumzia umuhimu wataalam wa misitu na kusema kuwa idadi yao haijitoshelezi kwa kuwa mpaka sasa hitaji la wataalam hao kwa nchi nzima ni 3000 ambapo kwa bajeti ya serikali ya mwaka huu imedhamiria kuajiri wataalam 500 wakati idadi ya wanaohitimu masomo hayo haitoshi.
Mhandisi Makani ametumia fursa hiyo kuwataka wahitimu hao kujenga tabia ya kutafuta namna ya kujiajiri ili kujenga fursa pana ya ajira kwa wataalam wengine wanaozalishwa katika vyuo mbalimbali.