Alhamisi , 15th Sep , 2022

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia  Omary Kipanga amesema serikali ina mpango wa kugawa Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kwa walimu wote kwa lengo la kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji

Akijibu maswali ya wabunge leo Jijini Dodoma Naibu Waziri Kipanga amesema kutokana na idadi ya vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa kuwa ndogo na haitoshi, wizara hiyo imeamua kuongeza vingine ili kutosheleza walimu wote nchini

"Vishikwambi vilivyotumika katika zoezi la sensa ni zaidi ya laki mbili na elfu tano, lakini sisi kama wizara tumeongeza vishikwambi vingine zaidi ya laki moja, kwahiyo niwaondoe hofu kwamba idadi ya vishikwambi ambavyo wizara imeratibu na kununua vitatosheleza kwa walimu wetu wote"